Jumuiko la Wanawake Tukuyu 2025.
Heshima kwa Mwanamke! Ndio kauli tunayoweza kuitumia kuisemea siku ya Jumamosi, Mei 10, 2025 baada ya wanawake Zaidi ya 1000 wakiungana na kina baba kupata elimu ya utunzaji fedha, ujasiriamali na uzoefu katika Maisha ya mwanamke wa Tanzania. Hayo yamefanyika katika jumuiko la wanawake lilioandaliwa na taasisi ya SHE CAN FOUNDATION lililofanyika Kivanga Garden, Kyimo Juu, Tukuyu.
Taasisi hiyo ambayo mwanzilishi na mkurugenzi wake ni mheshimiwa Sophia Hebron Mwakagenda, mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya inajihusisha na kutoa fursa mbalimbali za mafunzo kwa wasichana na wanawake kutoka kaya masikini.
Jumuiko la Wanawake wa Tukuyu lililenga pia kuwakusanya Pamoja wanawake kutoka maeneo mbalimbali na lilichagizwa Zaidi na uwepo wa taasisi za fedha zikiwemo benki za CRDB na NMB ambao ndio waliosimamia utoaji wa elimu ya utunzaji wa fedha kwa washiriki.
Hakika mama ni mshindi.
Mwakagenda akiwa amezungukwa na baadhi ya akina mama na akina baba kumpongezakwa kuwapatia mafunzo hayo.
Mwakagenda akizungumza wakati wa mafunzo hayo.



.jpeg)

Comments