L
Ouagadougou, Burkina Faso – Serikali ya Burkina Faso Chini ya Rais Ibrahim Traore imetangaza kuwa wazee hawatalazimika tena kulipia huduma za umeme na maji. Tangazo hilo limetolewa na Kiongozi wa mpito wa nchi hiyo, Ibrahim Traore, ambaye amesema kuwa huduma hizo zitakuwa bure kwa wazee wote nchini humo.
Kwa mujibu wa Traore, mpango huu ni sehemu ya juhudi zake za kuhakikisha ustawi wa wananchi, hususan wazee, na kuondoa mzigo wa gharama za maisha kwa watu waliotumikia taifa kwa muda mrefu. Aliongeza kuwa dhamira yake ya baadaye ni kuhakikisha kuwa huduma hizo zinapatikana bure kwa watu wote nchini Burkina Faso.
“Kila mtu anapaswa kuwa na haki ya kupata maji safi na umeme. Hizi ni huduma za msingi ambazo watu hawapaswi kulipia,” alisema Traore.
Mpango huo umepongezwa na wananchi wengi wa Burkina Faso na wadau wa haki za binadamu kama hatua chanya ya kijamii na kiuchumi.๐
Comments