Ridh

Nimekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Nchi ya Uswisi nchini Tanzania, Nicole Providoli, katika Ofisi yetu,jijini Dar es Salaam  Mei 16, 2025 alipofika kujitambulisha.

Katika kikao hicho, nimemshukuru Ndg. Balozi kwa ushirikiano uliodumu wa zaidi ya miaka 63 baina ya nchi zetu mbili na kumuhakikishia kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua mchango mkubwa wa Serikali ya Uswisi kupitia shirika la Swiss Aid na ushirikiano unaoendelea katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya afya, maendeleo ya jamii pamoja na masuala ya ukuzaji ujuzi kwa vijana.

Kwa upande nimepongeza na kuushukuru  ubalozi wa Uswisi kwa mchango wake katika kufanikisha kukamilika Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana (2007), Toleo la Mwaka 2024 ambayo inatoa mwongozo kwa vijana na wadau wengine kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi; na utayari wao kusaidia usambazaji wa Sera hiyo kuwafikia Wadau.







 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA