WAZIRI KIKWETE:SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA USTAWI WA WATU WASIOONA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu- Mhe.Ridhiwani Kikwete, amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuimarisha Ustawi wa watu wasioona nchini, hususani katika upande wa elimu, afya miundombinu, ajira pamoja na ushiriki wao katika nafasi za kiuchumi kwenye jamii. 

Mhe. Kikwete amebainisha kuwa serikali imeendelea kuimarisha ustawi wa watu wa wasioonakwa kuwapatia fursa za kuajiriwa, ujumuishwaji katika masuala ya TEHAMA, uboreshaji wa miundombinu ya elimu, uwezeshaji kupitia mikopo ya wajasiriamali na upatikanaji wa vifaa saidizi.

Ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha wasioona Tanzania (TLB) ofisini kwake jijini Dodoma. 

Amesisitiza kuwa serikali tayari inao Mkakati wa teknolojia Saidizi na Mfumo wa kielektroniki wa Taarifa na Kanzidata ya Watu wenye Ulemavu (PD-MIS) ambao unasaidia Serikali kupanga mipango ya huduma wezeshi kwa watu Wenye Ulemavu nchini wakiwemo watu wasiiona.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TLB mkoani Shinyanga Marco Mashauri, ameishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha ustawi wao kupitia TLB ambalo ni jukwaa la wasioona linalowawezesha kukutana, kuweza kujieleza,kuielimisha jamii juu ya uwezo wao, na mahitaji yao katika nyanja zote za maisha.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA