NJEZA ATOA SALAMU BUNGENI KUWAPA POLE WAFIWA, MAJERUHI AJALI YA MBALIZI


 Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza ametoa salamu za pole kwa waliofariki na majeruhi wa ajali iliyotokea katika Mlima Iwambi Mbalizi mkoani Mbeya Juni 7, 2025.

Ametoa salamu hizo za pole wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni Dodoma Juni 9, 2025, alipokuwa akiuliza swali kwa niaba ya Mbunge wa Viti Maalumu, Suma Ikenda.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali mbaya iliyotokea usiku wa tarehe 7 Juni 2025, mlima Iwambi Mbalizi na kusababisha vifo vya wananchi 28 na majeruhi 8." 

"Natoa pole kwa wafiwa wote na naungana na familia za marehemu na wote walioguswa na msiba huu mkubwa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi." 

Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape majeruhi wote nafuu ya haraka, na azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, AMEN.

Oran Manase Njeza (MB)
Mbunge Jimbo la Mbeya Vijijini
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MSIMAMIZI MKUU KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA