Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema kuwa wale wote wanaofanya makosa mtandaoni wakae wakijua kuwa ni kosa la kijinai ipo siku watakumbwa na mkono wa sheria. Ametoa onyo hilo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu maendeleo mbalimbali yanayoendelea nchini, katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya jengo jipya la wizara kwenye Mji wa Kiserikali wa Mtumba Makao Makuu ya Nchi Dodoma Juni 11, 2025.IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203

Comments