YANGA YAFANYA MABADILIKO, YAFUTA SAFARI YA RWANDA

 


KLABU ya Yanga SC imetangaza kufanya mabadiliko kwenye ratiba yake ya mwisho wa msimu, ikitangaza kufuta safari ya kuelekea Rwanda ambako walitarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports mnamo Juni 15. Uamuzi huu umechukuliwa kwa lengo la kuelekeza nguvu zote kwenye mechi tatu muhimu za kumaliza msimu wa 2024/25.


Kwa mujibu wa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe, safari hiyo sasa imeahirishwa hadi kipindi cha maandalizi ya msimu ujao wa 2025/26 (pre-season), ambapo klabu hiyo itapanga upya ratiba yake ya michezo ya kirafiki.


Kamwe amesema Yanga kwa sasa inajikita kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji, pamoja na fainali ya Kombe la CRDB dhidi ya Singida Big Stars.


Aidha, Kamwe amefafanua kuwa kikosi cha Yanga kitasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Mbeya mnamo Juni 15, kwa ajili ya maandalizi ya mechi dhidi ya Tanzania Prisons itakayochezwa Juni 18. Timu hiyo itatumia siku mbili kujiandaa na mchezo huo muhimu wa ligi.


Wakati huo huo, Yanga imesisitiza kuwa haitocheza mechi ya Ligi Kuu namba 184 dhidi ya Simba SC, iliyopangwa kufanyika Juni 15, hadi pale Bodi ya Ligi itakapotoa maamuzi rasmi kuhusu malalamiko yao juu ya mchezo huo ambao awali ulitarajiwa kuchezwa Machi 8.


U

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA