BENDERA YA NCHI YETU ENZI TUNAITWA DEUTSCH-OSTAFRICA.


 

- Hii ndio ilikuwa Bendera yetu, Na Katikati ya bendera ni Ngao ya Jamii (Coat of arms) ya Nchi yetu enzi tunaitwa Deutsch-Ostafrika (Ujerumani ya Afrika Mashariki) miaka ya 1885 mpaka 1918.


- Wakati huo nchi ilikuwa na Eneo la Mita Square 994,996 Km² ndani yake kuna Burundi na Rwanda, na Eneo la Nchi ya Msumbiji lililoitwa Kionga Triangle.


- Yaani Kiufupi eneo la Nchi yetu lilikuwa kubwa mara tatu ya Eneo la Ujerumani Inayotutawala.


- Katika Kipindi hicho Nchi yetu Ilibadili Mji mkuu mara tatu, Ulianza Bagamoyo (1885–1890) Ikaja Dar es Salaam (1890–1916) Mwishoni ikaja Tabora (1916) ambao ulikua mji mkuu kwa Muda.


- Hapa Lugha Rasmi ilikua Ni Kijerumani, Hizo Kiswahili, Kirundi,Kiarabu Kinyarwanda Zilikua zikihesabika kama lugha Pori tu.


- Unachotakiwa Kufahamu Ujerumani ilianzisha programu ya elimu kwa Waafrika iliyojumuisha shule za msingi na sekondari (Elementary schools) na vyuo vya ufundi (Vocational Schools) Wajerumani waliweka mpangilio kuanzia Sifa za mwalimu, mitaala ya Elimu, vitabu vya kiada, nyenzo za kufundishia, Vitu vyote hivyo vilikidhi Kiwango ambacho hakikulinganishwa popote katika bara la Afrika nchi za Kitropiki, 


- Hayo Ya Kwamba Tanganyika Ilikua Bora kwenye Swala la nyenzo za Elimu sio maneno Yangu, Subiri Nikwambie, Mwaka 1924  Miaka Kumi baada ya Vita Ya Kwanza ya Dunia Kuanza, Ambapo Pia ilikua Miaka 6 ya Uingereza Kuitawala Tanganyika, Jamaa mmoja wa kuitwa Phelps Stokes kutoka Marekani aliitembelea Tanganyika, Alipofika na Kukaa kwa muda alisema wazi "Kuhusu Elimu, Wajerumani wamefanya maajabu, Miaka kadhaa lazima ipite kabla ya elimu kufikia kiwango iliyokuwa imefikia chini ya Wajerumani."


- Hata Neno La Kiswahili "SHULE" limetoka kwenye Neno la Kijerumani "SCHULE" yote yakimaanisha "SCHOOL"


- Maeneo Mengi yalikua na Majina ya Kijerumani, sema historia haifundishi kuyajua, Mfano:

• Rombo iliitwa Fischerstadt

• Nyakanazi iliitwa Friedberg

•Kisarawe Iliitwa Hoffnungshรถh

•Tukuyu iliitwa Langenburg

•Ushetu iliitwa Marienthal

•Shume (Huko kwa Wapare) kuliitwa •Neu-Hornow

•Mbulu Kuliitwa Neu-Trier

•Sekenke Paliitwa Sachsenwald na ilikua ni Mgodi.

*•Manda ilitwa* Wiedhafen

•Lushoto iliitwa Wilhelmsdorf.


- Kipindi hiki ndio Tulijengewa Reli iliyoitwa Usambara Railway mwaka 1891 Ilijengwa na Wajerumani na ilikua na Km 350, Ilianzia Mjini Tanga, Ikawa na Makutano Na Kenya Mji wa Kahe, Ikapita Moshi mpaka Arusha.


- Wajerumani Katika Reli hii walikua na Vichwa vya Treni 18 (Locomotive) na mabehewa 199, Kipindi hicho Reli hii ilikua na Wafanyakazi 562 huku kati yao 35 tu ndio Walikua Wajerumani.


- Lengo la Wajerumani kujenga Reli hii ilikua ni Kuunganisha Bandari ya Tanga na Ziwa Victoria kupitia milima ya Usambara.


- Treni ya Kwanza Lilipita Likiwa Tupu Tarehe 26 September 1911 ili kujaribu Safari na Kufanikiwa 100%, Likapita tena likiwa na Abiria Tarehe 4 October 1911 na kufanikiwa 100%  Wajerumani wakaamini Kweli Kitu ni Konki, Hivyo ukafanyika uzinduzi wa Reli Tarehe 7 February 1912, Na Baada ya Hapo Treni lilikua lazima lifanye safari Kila siku Kutoka Tanga mpaka Buiko na Kurudi, Safari ilichukua Muda wa saa 14 na dakika 40. Reli hii haikukamilika Mpaka Arusha sababu ya  Vita ya Kwanza ya Dunia, Waingereza ndio Wakaiunganisha.


Na Mhe. DC Kundya Mwangi

*#Copy and paste*

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA