China ni Taifa lenye watu Imara sana na wenye heshima Popote wawapo Dunaini, Kuna watu Wameniuliza Inakuaje Washirika wa China, ukitokea mgogoro wa ndani katika Nchi yoyote mshirika wa China hua china inaondoka katika Eneo hilo bila kutoa msaada wa kijeshi?
Mfano: Sudan Darfur ni mshirika Mkubwa wa China ila Baada ya migogoro ya wao kwa wao, China Imeondoka Nchini Sudan kiasi kwamba Wengine wanachukulia kua China ni Dhaifu.
Kwakua mimi Chotara Mweusi Sultan ndio Profesa wa Uchambuzi wacha Niwapeni Elimu kuhusu hilo Muelewe China Na sera zake za Mambo ya Nje.
Sera ya China ya kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine Yani non-interference ina mizizi ya kihistoria, kimkakati na kiitikadi.
China ilipitia karne ya fedheha ๐Century of Humiliation kuanzia karne ya 19 hadi katikati ya karne ya 20, ilipovamiwa, kugawanywa na kudhibitiwa na mataifa ya Magharibi na Japani.
China ilijifunza kuwa kuingiliwa kwa mambo ya ndani ni chanzo cha kudhoofisha taifa. Ndiyo maana๐
๐Inapinga vikali uingiliaji wa nje
๐Inaheshimu mamlaka kamili ya taifa
Tangu 1954, sera ya nje ya China imejengwa juu ya kanuni Kuu tano๐
1๐Kuheshimiana kwa mamlaka ya kitaifa
2๐ Kutokuingilia mambo ya ndani
3๐Kutokushambuliana
4๐Usawa na manufaa ya pande zote
5๐Kuishi kwa amani
Kanuni hizi ndizo msingi wa mahusiano yake na Afrika, Asia na Amerika ya Kusini. Maslahi ya kiuchumi, Biashara bila masharti ya kisiasa
China inaamini kuwa ๐Kila taifa lina njia yake ya maendeleo
๐Demokrasia au mfumo wowote wa utawala si sharti la biashara
Tofauti na Marekani au Ulaya ๐huambatanisha biashara na masharti ya kisiasa kwa Mgongo wa demokrasia na haki za binadamu
China Inatoa mikopo na uwekezaji bila masharti ya Kuingilia mambo ya ndani ya Nchi yoyote Yani Kama mtagombana Nyie kwa nyie sio jukumu la China kuingilia upande wowote katika mgogoro wenu wa ndani Zaidi mjitafakari na mjenge Nchi Yenu.
Sera kama Hii ya China huwafanya washirika wake wengi wajisikie huru na kuheshimiwa
China inahitaji sana Kuepuka kurudia kile ilichokipinga, China huona uingiliaji wa kijeshi au kisiasa kama๐
๐Ubeberu mpya Waingereza wanaita neo-colonialism
๐Njia ya mataifa makubwa kudhibiti rasilimali za wengine
Hivyo basi๐ “Hatufanyi kwa wengine kile tulichofanyiwa.” sera ya China.
China hujenga Mkakati wa muda mrefu wa ushawishi wa kimya China haingilii Sera ya mambo ya ndani ya Nchi yoyote, lakini
๐Huongeza uwepo wa kiuchumi
๐Huunda utegemezi wa kibiashara
๐Hujijengea ushawishi wa muda mrefu bila vita
Ushawishi huu ni wa kiuchumi, si wa kijeshi wala kisiasa moja kwa moja. Sababu ya ndani ya China yenyewe China ina
๐Xinjiang
๐Tibet
๐Hong Kong
๐Taiwan
Ikiwa ingeruhusu kuingilia Sera ya mambo ya ndani ya mataifa mengine, Ingehalalisha mataifa hayo kuingilia masuala yake ya ndani
๐Kwa hiyo inalinda sera hii kwa maslahi yake binafsi. Unajisikiaje Jirani yako anakuja kuingilia Ugomvi wako wewe na mkeo Alafu anakaa upande mmoja? Yani anampa nguvu mkeo alafu wewe anakubeza ? China haipendi hivo inaamini Kwamba Waathirika si majirani bali ni ninyi wenyewe.
Huu ndio Mtazamo wa China juu ya migogoro ya ndani China huamini๐
๐Migogoro ya ndani lazima itatuliwe na wenyewe
๐Mazungumzo ya ndani ni bora kuliko shinikizo la nje
Ndiyo maana mara nyingin Hupiga kura ya kujizuia kwenye Baraza la Usalama la UN, Hupendelea diplomasia tulivu badala ya adhabu au vikwazo
Baki na Mimi kwa Mengi zaidi yanayo jiri Duniani
By Professor Chotara Mweusi Sultan kutoka viunga vya ๐
๐Sharif shamba
๐Ilala Dar es salaam
๐Tanzania
Bingwa la uchambuzi wa maswala ya kijamii, Uchumi na Siasa za Dunia Yetu.

Comments