TANZANIA, MAREKANI KUIMARISHA USHIRIKIANO



Serikali ya Tanzania na Marekani zimekubaliana kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia, ikiwa ni mwendelezo wa ushirikiano wa muda mrefu baina ya mataifa hayo.

Hatua hiyo, imefikiwa wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo nchini humo alikokutana na viongozi mbalimbali wa Marekani.

Balozi Kombo ameanza ziara hiyo leo, Jumatatu Desemba 15, 2025 na kukutana na viongozi mbalimbali wa bunge na Serikali ya Taifa hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Tanzania mjini Washintong, Serikali hizo zimekubaliana mambo kadhaa ya uimarishaji mahusiano hayo.

Pia, Kamati ya Bunge la Marekani, imepokea mwaliko wa kufanya ziara rasmi nchini Tanzania mapema iwezekanavyo.

Miongoni mwa viongozi aliokutana nao ni Mbunge wa Florida kupitia Chama cha Republican, Brian Mast, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Wawakilishi la Marekani.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA