Kwanza Inatupasa Kufahamu zama zimebadilika mikakati ya Kuwakataa Wanyonyaji Inaendelea Afrika nzima kwasasa Tahadhari ni kubwa sana kwa Nchi za Magharibi Husasa Nchi kama ya Umoja wa majimbo (Marekani)
Marekani hupendelea kufanya kazi na mataifa Imara yani ๐stable nations
Fahamu kua Sera ya nje ya Marekani inatoa kipaumbele kwa๐
๐Utulivu wa kisiasa
๐Utabiri wa sera Yani policy predictability
๐Mazingira rafiki kwa uwekezaji
๐Utawala wa sheria na uhuru wa kiuchumi
Kama Mnavyo Fahamu Tanzania imekuwa Muhimili wa utulivu katika Ukanda wa Afrika Mashariki kwa miongo Na Miongo. Hili linaiweka Tanzania kwenye kundi la nchi ambazo Marekani na nchi za Magharibi hutaka kulinda mahusiano nao kuliko kuyavuruga.
Inatakiwa Tufahamu Kwa nini Marekani haiwezi kuruhusu uhusiano na Tanzania kuharibika, Tanzania ina umuhimu wa kimkakati yani strategic importance kwa sababu๐
๐Ni kitovu cha kijiografia Afrika Mashariki.
๐Ina rasilimali muhimu kama gesi, madini. muhimu kwa teknolojia, nishati.
๐Ni lango la kibiashara kwa SADC na EAC.
๐Ina bandari muhimu ya Dar es Salaam na Bagamoyo.
๐Ni nchi yenye utulivu wa kijamii na kisiasa.
๐Ni Nchi isio Yumbishwa Katika sera zake za mambo ya ndani.
Kwa Marekani, kupoteza ushawishi Tanzania kungekuwa na madhara makubwa sana kama๐
๐Kupoteza Mshirika muhimu
๐Kuipa Nafasi Zaidi China na Urusi.
๐Kuporomoka kwa ushawishi wa Magharibi Afrika Mashariki, hususa wakati China na Urusi wanaimarisha uwepo wao Kwa Kasi na nguvu nyingi.
Ziara ya Kaimu Balozi wa Marekani Ikulu na Mazungumzo Na Mh Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhusu “mabilioni” Hii inaonyesha mambo mawili makubwa
๐
๐Marekani imepokea ujumbe wa Tanzania wa kutaka usawa (win–win)
Hotuba ya Rais iliyo na kauli kama “Who are you?” iliwafikisha moja kwa moja Wamagharibi kwamba
๐
๐Tanzania haitakubali tena mikataba ya kinyonyaji.
๐Hakutakuwa na ubabe wa kiuchumi.
๐Ushirikiano lazima uwe wa maslahi ya pande zote.
Badala ya kukasirika kwa Kauli hiyo, Marekani imechukulia kauli hiyo kama.
๐
๐Ukweli wa kisera, sio matusi.
๐Onyo la kidiplomasia kwamba zama za "take it or leave it" zimepitwa na wakati.
๐Ishara ya kwamba Tanzania sasa inajiamini kimataifa.
Marekani haitaki kupoteza nafasi zake kwa China au Urusi Kitu ambacho Marekani imewahi Mapema kujisalimisha Yani Kuingia Ikulu kwa mazungumzo ya kiwango cha mabilioni kunaonesha kwamba
๐
๐Wanaokoa nafasi zao kabla haijachukuliwa na mataifa mengine.
๐Wanaonesha kuwa bado wapo tayari kushindana kwa ustaarabu.
Athari ya Uwepo wa Urusi Tanzania Hili ndio sehemu muhimu zaidi ya geostrategy Uwepo wa Urusi (uwekezaji, mafunzo, nishati, usalama) unasababisha
๐
๐Marekani na Magharibi kuongeza uwazi katika mikataba.
๐Kupungua kwa masharti ya kibeberu
๐Ushindani wa kimaendeleo ambao Tanzania inanufaika nao
๐Majadiliano kuwa ya heshima zaidi, si ya kulazimisha
Kwa maneno mengine Tunasema kwamba
๐Tanzania imeongeza "bargaining power".
Tanzania kama Taifa la Kimkakati Ukanda wa Afrika mashariki na Nchi za Maziwa makuu Bila kusema kubwabwaja ukweli ni huu
๐
๐Tanzania sasa haipigiwi debe kama nchi dhaifu ya kutegemea misaada.
๐Ni mchezaji muhimu katika usalama wa Afrika Mashariki, madini muhimu (helium, graphite, nickel), na njia za biashara.
Tazama Dunia inavyogawanyika upya yani East vs West, Tanzania imeendelea chukua msimamo wa non-alignment ya kisasa zaidi.
๐
๐Inafanya kazi na Marekani
๐Inaendelea na China
๐Inafanya kazi na Urusi
๐Inashirikiana na Mataifa ya Ghuba Uwajemi na Asia
Hii ni diplomasia ya "Rarafiki wa wote, Asie na Adui" Sera ambayo mataifa mengi makubwa wanaiheshimu. ๐"Win–Win Situation” ndiyo msingi wa uwezo wa Tanzania kwasasa Atakae na aje.
Tanzania Ya sasa haiendi Washington au Moscow kama Omba Omba bali kama
๐
๐Nchi yenye rasilimali
๐Soko la watu milioni 70+
๐Kituo cha utulivu
๐Mlango wa uchumi wa kikanda
๐Nchi inayojitegemea kimkakati
Kwa hiyo Magharibi wanakuja kwa msimamo wa๐
๐Kusikiliza
๐Kutiwa hofu kidogo
๐Kutaka kulinda maslahi yao bila kupoteza ushawishi
Ifahamike kwamba baada ya Nchi Nyingi za Magharibi Kupoteza Ushawishi wao Ukanda wa Sahel na Kusini mwa Afrika Kumeifanya Tanzania ikae kwenye kipindi cha historia ambacho๐
๐Ushawishi wake unaongezeka kimataifa.
๐Mamlaka yake ya majadiliano imeimarika.
๐Mataifa makubwa yanashindana kwa heshima kutaka ushirikiano na Tanzania.
Kauli za uthubutu kutoka kwa viongozi, ikiwemo “Who are you?”, zimewafanya Magharibi kutambua kuwa zama zimebadilika Sio kila Homa ni Malaria zinge Ni kaswende.
Huu ndio msingi wa kuwa taifa la kimkakati, na Tanzania kwa sasa iko hapo katikati ya nguvu mbili kubwa duniani Yani West na East, ikicheza mchezo wake kwa ustadi.
Nimalize kwa kusema Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania wabariki Viongozi wetu na Utubariki watanzania wote.
Baki na Mimi kwa Mengi zaidi yanayo jiri Duniani
By Professor Chotara Mweusi Sultan kutoka viunga vya ๐
๐Sharif shamba
๐Ilala Dar es salaam
๐Tanzania
Bingwa la uchambuzi wa maswala ya kijamii, Uchumi na Siasa za Dunia Yetu.

Comments