NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA NDUGU JOHN MONGELLA ASIKILIZA KERO NA MAONI YA MABALOZI JIJINI MWANZA



Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Ndugu John Mongella, amesikiliza kero na maoni ya Mabalozi kutoka Wilaya za Ilemela na Nyamagana, katika mkutano uliofanyika leo tarehe 04 Februari, 2026, katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Mwanza.

Akizungumza katika mkutano huo, Mongella aliwapongeza Mabalozi kwa michango na maoni yao mazuri ya kukijenga Chama kuanzia ngazi ya Shina, huku akisisitiza umuhimu wa Mshikamano, Uwajibikaji na Uadilifu katika utekelezaji wa majukumu ya Chama katika maeneo yao.

Aidha, Mongella aliahidi kushughulikia changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na Mabalozi, ikiwemo kuwawezesha vitendea kazi kwa Mabalozi ili waweze kuwa na ufanisi katika utendaji kazi wao na kuimarisha mawasiliano na Wanachama.

Mkutano huo umefanyika katika hali ya utulivu na mshikamano, ukiakisi dhamira ya Chama Cha Mapinduzi ya kusikiliza maoni ya Wanachama wake na kuendelea kusonga mbele kwa Umoja na Amani.

“Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.”


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MIKOA 10 YENYE KIPATO KIKUBWA ZAIDI KWA MTU MMOJA MMOJA

BODABODA ALIPWA PIKIPIKI BAADA KUSAFIRI KWA BODA KWA SAA 10 MBEYA HADI DAR

ASANTE GWIJI YAYA TOURE KWA KUPASUA UKWELI UKWELI KUPENDELEWA KWA MOROCCO

CONFIRMED HAWA NDIO WACHEZAJI WETU 12 WA KIGENI 🦾

'MAREKANI IKIJARIBU KUANZISHA VITA NA URUSI ITAANGAMIA'

RAIS WA SENEGAL AWAPATIA ZAWADI NONO WACHEZAJI WALIOFANIKISHA UBINGWA WA AFCON 2025

NYOMI YA WASENEGALI WAKISHANGILIA UBINGWA WA AFCON 2025

MAREKANI YAITEKA MELI YA MAFUTA YA URUSI IKITOKEA VENEZUERA