VIONGOZI WA UWT WAMLILIA MUNDE TAMBWE

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Mary Pius Chatanda (MCC) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa (UWT) Mhe. Zainab Shomari (MNEC) ametoa pole kwa Familia ya Marehemu Munde Tambwe, Waombolezaji, na  UWT kwa ujumla na kusema kuwa tumempoteza mpiganaji mwenzetu aliyetumainiwa katika utendaji kazi,  Binti mashuhuri na aliyekuwa mfano mzuri aliyeigwa na Vijana wengi, 


Marehemu Munde alikuwa ni kijana aliyejipambanua katika nafasi yake ya Uongozi, Alikuwa mstari wa mbele kushawishi vijana wenzake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali Pamoja na Ubunge wa Majimbo na Viti Maalum, hivyo kifo chake ni pigo kubwa kwetu sisi UWT, na tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa Amani.

Marehemu Munde Tambwe amezikwa leo tarehe 04 Februari, 2026, katika Makaburi ya Kidongo Chekundu kata ya Ngambo Mkoani Tabora, huku viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakihidhuria msiba wake.






 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MIKOA 10 YENYE KIPATO KIKUBWA ZAIDI KWA MTU MMOJA MMOJA

BODABODA ALIPWA PIKIPIKI BAADA KUSAFIRI KWA BODA KWA SAA 10 MBEYA HADI DAR

ASANTE GWIJI YAYA TOURE KWA KUPASUA UKWELI UKWELI KUPENDELEWA KWA MOROCCO

CONFIRMED HAWA NDIO WACHEZAJI WETU 12 WA KIGENI 🦾

'MAREKANI IKIJARIBU KUANZISHA VITA NA URUSI ITAANGAMIA'

RAIS WA SENEGAL AWAPATIA ZAWADI NONO WACHEZAJI WALIOFANIKISHA UBINGWA WA AFCON 2025

NYOMI YA WASENEGALI WAKISHANGILIA UBINGWA WA AFCON 2025

MAREKANI YAITEKA MELI YA MAFUTA YA URUSI IKITOKEA VENEZUERA