.Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako, Machi 12, 2026 wamewasili mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya kukagua Maendeleo ya Miradi chini ya Wizara ya Ujenzi.
Mara baada ya kuwasili, wajumbe hao wamepokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa Dkt. Mussa Ali Mussa, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa.
Katika ziara hiyo, kamati imepokea Taarifa na kukagua maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa jengo la Taaluma katika Chuo cha Teknolojia ya Ujenzi (Institute of Construction Technology – ICoT).
Kamati imeeleza kuridhishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo, ambapo imebainishwa kuwa hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 74 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2026.
Ziara hiyo pia imehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde, pamoja na watendaji wengine wa wizara.







Comments