KUTUNZA MAZINGIRA NI IBADA, PANDENI MITI -BALOZI WA MAZINGIRA SINENE

 Balozi wa Mazingira,Ahidi Sinene ametoa wito kwa wananchi kuzitumia mvua za masika zinazoendeleo kupanda miti kwa ajili ya kuhifadhi mazingira na kwani jambo hilo ni ibada kama ibada zingine na kwamba kutotunza mazingira ni dhambi kama zilivyo dhambi zingine.


Ameyasema hayo aliposhiriki pamoja na wanafunzi na walimu kupanda miti zaidi ya 100 aliyoitoa katika Shule ya Sekondari Umonga jijini Dodoma Machi 16, 2026.

Kila anapokwenda kupanda miti amekuwa Sinene akihamasisha kila mwananchi kuwajibika kupanda angalau kwa uchache miti mitano katika eneo lake kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani.
Balozi huyo wa Mazingira ambaye pia ni Mjumbe mstaafu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodpoma, amekuwa na tabia kupanda miti katika maeneo mbalimbali mkoani humo ambapo Januari 16, 2021, Sinene alikwenda kushiriki kupanda miti katika Shule ya Sekondari Bihawana, Kata ya Mbabana nje kidogo ya Jiji la Dodoma ambapo walipanda miti 230 ikiwemo ya matunda.
Balozi wa Mazingira,Ahidi Sinene akipanda mti.


Wanafunzi wa shule hiyo wakishiriki kupanda miti.




 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA -0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

IRAN YAMTANGAZA AYATOLLAH MPYA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

Wasifu wa Kizza Besigye

KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

KWA NINI MAASKOFU JANA KWENYE IBADA YA KUMUAGA PENGO WALIVAA MAVAZI MEUPE WAKATI NI MSIBA..?

DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025

WANAOTAZAMWA KUMRITHI AYATOLLAH ALLY KHAMENEI.

MATUKIO RAIS, AMIRI JESHI MKUU DKT. SAMIA AKIZINDUA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA (MMUT)